Pambano la ndondi
lililokuwa limepangwa kufanyika kati ya rapa DMX na George Zimmerman
limetangazwa kuwa halitokuwepo tena, ikiwa ni siku nne kabla ya
kufanyika kwa mkutano rasmi na waandishi wa habari kutambulisha
pambano.
Taarifa hizi zimetangazwa
na promota aliyekuwa anaandaa pambano hili, Damon Feldman na
afisa habari wa DMX, Domenick Nati na hii ni kutokana na mpambano huu
kupata
pingamizi nyingi kutoka kwa watu hususan kutokana na Zimmerman
ambaye umaarufu wake umetokana na tuhuma za mauaji
ya mtu mweusi.
No comments:
Post a Comment