"Nataka kuwashinda wengine wote", ndiyo
yalikuwa maneno ya mwisho ya Isaac Richardson kijana mdogo mwenye
umri wa miaka 20 aliyejiingiza katika shindano katika mtandano ikiwa
ni shinikizo la marafiki, lililomtaka anywe mchanganyiko wa pombe
kali ikiwa ni pamoja na mvinyo na bia.
Mchezo huu ujulikanao kama
NekNomination uliopo Facebook, ni mchezo wa kunywa pombe kali, ambao vijana tofauti
hutuma picha za video katika mitandao wakionyesha au wakifanya tambo
ya michangayiko mbali mbali ambayo wameweza kuinywa. Vijana hawa
wanakunywa michanganyiko ya ajabu ajabu ya pombe halafu wanawataka
wenzao kwingine duniani wafanye zaidi ya wao kama wataweza.
Kijana Isaac Richardson ambaye bni
muhudumu wa hote;li ya kifahari huko Uingereza aliwaambia wenzake
anataka awashinde wengine wote waliowahi kushiriki mchezo huo.
Isaac amekuwa muingereza wa kwanza kufariki katika mchezo huo, huku kukiwa na taarifa za wengine wawili
kufariki nchini Ireland kwa mchezo wa aina hiyo.
Muhudumu huyu wa hoteli
alipoteza
fahamu dakika chache baadaya kunywa mchanganyiko huo na alipofikishwa
hospitali alikwisha fariki dunia.
Mchezo huu ulianza nchini Australia
mwezi uliopita sasa umesambaa kote duniani.
Maelfu ya vijana sasa Ulaya wanafanya
majaribio ya aina hii kwanzia iliyo hatari zaidi mpaka inayotia
kinyaa.
Mama mzazi wa Richard alishikwa na
mfadhaiko wa ajabua laiposikia habari z amwanae kufariki dunia kiasi
kwamba alishindwa kuzungumza.
Wazazi, walezi pamoja na makundi ya
jamii Ulaya yameutaka mtandao wa kijamii wa Facebook kufutilia mabali
mchezo huo kwani unapa mshawashawa viajna wa kutaka kujiingiza na
kushiriki na pale mshindi anapotafutwa, mtu anakuwa na uwezo wa
kujaribu jambo lolote.
Wazungu
wanasema Curiousity Killed the Cat.
Hata
kama ni kwa nchi Iliyo endelea....Ivi kweli kuna haja ya kufanya
mambo kama haya?...
No comments:
Post a Comment