Tatto Mpyaaa ya Chameleone ... Ona alichochora...
0
Jose Chameleone, Staa wa
muziki wa nchini Uganda katika kuonyesha upendo mkubwa alionao kwa
mke wake Daniella, ameamua kujichora tattoo ya mke wake huyu katika
shingo yake.
Mbali na kusherehekea sikukuu ya wapendanao, Chameleone ambaye tayari
ana tattoo za majina ya watoto wake wote katika mkono wake, amefanya
hivi katika kum
thibitishia mama watoto wake kuwa, mbali na watoto
wake, yeye pia ni mtu mwingine mwenye nafasi kubwa katika moyo wake.