Waokoaji wa dharura nchini Afrika ya kusini hiyo jana walikuwa
katika heka heka kutaka kuokoa wafanyakazi 9 wa mgodini ambao bado
hawakuonekana katika mgodi uliokuwa ukiungua moto magharibi mwa jiji
la Johannesburg.
Wamiliki wa mgodi huo, Harmony Gold walisema kuwa juhudi za kuokoa
hao walioumizwa zilikuwa zikiyumbishwa na moshi mkali uliokuwa ukitoka baada ya kuporomoka kwa miamba. 9 kati ya wafanyakazi 17 ambao awali walikuwa wamekwama ndani ya
mgodi huo bado ya wengine nane kuokolewa mapema hiyo jana.
Moto huo ulizuka umbali wa kilomita 1.7 chini ya ardhi katika
mgodi wa Doorkop majira ya jioni ya juzi nainasemekana ilitokana na
tetemeko la ardhi. Inasemekana tetemeko hilo lilisababisha hitilafi ya umeme katik
amgodi huo kusababisha moto ambao mpaka wakati wa uokoaji ulikuwa
ukiwaka.
Uongozi wa kampuni hiyo iliwaomba sana waokozi kufanya jitihada
kumaliza shughuli hiyo kwani hata mirija ya hewa safi ilikwisha pata
hitilafi.
Licha ya juhudi za kuhakikisha mazingira salama migodini,
bado
ajali nyingi zinaendelea kutokea nyingine zikisababishwa na uzembe. Zaidi ya watu 120
waliuwawa mwaka 2010. Kutafuta wachimbaji madini waliozama ndani ya
migodi imeendelea kuwa tatizo hata hivyo makampuni makubw ahutumia
mifumo maalumu kuhakikisha wanabaki salama huko chini.
Tarifa zinadai kuwa, Wawekezaji walipoambiwa kuhusu hili
hawakuonekana kuogopa au kushtushwa na taarifa hizo. Sekta ya madini ya dhahabu nchini Afrika kusini imezorota kiasi
fulani kwa miaka 40 iliyopita, kutoka kuwa nafasi ya kwanza duniani
kufikia ya sita
.
Afrika kusini ilizalisha takribani Kilo 167,235 za dhahabu mwaka
2012.
No comments:
Post a Comment