Baada ya mwaka 1995 Hili hapa jengo lingine kuporomoka huko S. Korea
0
Zaidi ya watu kumi wanasadikiwa kupoteza maisha na zaidi ya mia moja kujeruhiwa vibaya kufuatia
kuporomoka kwa jengo moja katika hoteli maarufu Korea ya Kusini.
Zaidi ya watu 560 walikuwa wakishirki
tamasha moja katika jiji la Gyeongju nchini humo sehemu ya hoteli ambapo jengo hilo liliporomoka.
9 ya waliouwawa walikuwa wanafunzi.
Maafisa wanadai kuwa wanafuzni wote waliobaki wako salama.
Vikosi vya Zima moto vimelalamikia hali
ya hewa, kuwa barafu iliyotanda katika paa za jumba hilo ndizo
zilizosababisha uzito katika jumba hilo kufuikia kuporomoka. Hali ya
hewa pia imeleta changamoto kubwa katika uokoaji.
Msemaji kutoka wizara ya Ulinzi na
uatawal wa Uma amesemakuwa watu kumi ndiyo waliothibitika kufariki na
101 kuumizwa vibaya. Vikosi vya uokoaji vimeendelea na
kuokoa watu wengine. Vyombo vya habari nchini humo vimedai
kuwa jengo hilo limeporomoka mida ya saa tatu usiku maajira ya huko
Wanafunzi wengi walikuwa katika hoteli
hiyo, na wengi walifanmikiwa kutoka katik ajengo hilo wenyewe.
Sehemu hii ya Korea kusini imekumbwa na
hali mbaya ya hewa, wiki nzima iliyopita. Jengo hilo limesemekana kuwa la kisasa
sana kuhimili vishindo, hata hivyo Polisi wamehoji kawanini Barafu
iliyotanda katika paa haikutolewa mara moja.
Jiji la Gyeongju ni jiji la kihistoria
lililokuwa mji mkuu wa falme moja ya zamani ya Korea na ni eneo kubwa la kitalii. Moja ya tukio la aina hii liliwahi
kutokea hukohuko Korea mnamo mwezi wa sita mwaka 1995, ambapo jengo
la kibiashara la Seoul la Sampoong Department Store lilianguka na kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Kumbe uzembe na huko pia????