NTAGANDA HAKUWA NA "OPTION" NDO MAANA ALIJISALIMISHA....
0
Kiongozi
wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda ambaye
alikuwa akiogopewa mno anafikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu wa Kivita (ICC), hii leo.
Muasi
huyo ambaye alishangaza Marekani mwaka jana baada kujisalimisha
kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Rwanda, sasa anakabiliwa na makosa
kadhaa yakiwemo ya ubakaji, mauaji na kutumia askari watoto.
Majaji
wa Mahakama hiyo iliyopo The Hague, Uholanzi wanasiku 60
za kuamua
iwapo Ntaganda anakesi ya kujibu, baada ya kuisikiliza shauri lake
kwa mara ya kwanza hii leo.
Ntaganda
ambaye alipewa jina la “The Terminator” alikuwa ndie muanzilishi
wa kikundi cha waasi cha M23, ambacho kilisambaratishwa na vikosi vya
Umoja wa Mataifa Novemba mwaka jana.
Ntaganda
alikuwa sehemu ya Umoja wa wazalendo waasi wa kundi liloongozwa
naThomas Lubanga ambaye mwishoni mwa mwaka jana alikuiwa mtu pekee
aliyetiwa hatiani an ICC.
Mashariki
mwa nchi ya kidemokrasia ya Kongo, kumekuwepo na miongo miwili ya
ghasia zilizotokana na itikadi za kikabila ambapo makabila hayo
yalikuwa yakipigania kutawala sehemu hiyo yenye madini ya thamani.
Ghasia
hizo zilianza pale ambapo kundi la wahutu lilituhumiw akuhusiak moja
kwa moja na ghasia na mauaji ya halaiki iliyotokea mwaka 1994. Kama
tu wale walioitawala Rwanda kwanzia mauaji yale ya kirambi Generali
Ntaganda ni Mtutsi.
Makundi ya haki za binadamu yalisherehekea Generali Gen Ntaganda's
alipojisalimisha, kama ushindi wa mahamaka na sheria ya kiamataifa na
pia ushindi kwa awaathirika wa vita.
Hata hivyo wadadisi wa kisiasa wanasema kujisalimisha kwake ni kama faid akwake kwani asinge jisalimisha angeuwawa, hivyo hii ni kama njia yake ya kubaki hai hata kama atafungwa.