Mrembo na staa wa muziki aliyekuwa mpenzi wa Justin
Bieber, Selena Gomez ameamua kuchukua tahadhari na kutafuta msaada
zaidi katika kituo cha kusaidia saikolojia na kurekebisha tabia
ambapo imefahamika kuwa tayari ametumia wiki mbili huko Arizona
Marekani akitibiwa ili kuweka mambo yake sawa.
Hatua hii ya Selena kutafuta msaada wa aina hii
imetajwa kuwa haihusiani kwa namna yoyote na shida ya dawa za kulevya
wala pombe, na lengo lake kubwa limetajwa kuwa ni
kutafuta msaada wa
kutawala hisia zake pamoja na kuwa na uwezo wa kusimamia na
kukamilisha mambo yake bila wasiwasi.
No comments:
Post a Comment