KRIS JENNER, BRUCE JENNER KUBAKI MARAFIKI LICHA YA KUTENGANA
0
Wenza hawa wenye mvuto mkubwa hasa kutokana na nafasi zao katika show ya maisha ya kila siku ya KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS wametangaza kutengana mapema wiki hii. Hata hivyo wapo wanaodhani kuwa mali walizokuwa nazo zitaleta shida katika kutengana kwao. Kwani kiasi cha Dola millioni 125 kinahusika..
Bruce mwenye umri wa miaka 63, ndiye aliyekuwa mwenye mali nyingi wakati wawili hawa walipokutana mwaka 1991 baada ya kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki pamoja na madili mengine mengi.