MZOZO WA BAJETI MAREKANI WACHUKUA SURA MPYA
0
Rais wa marekani Barack Obama amekiri
kuwa yupo tayari kufanya majadiliano na wajumbe wa chama cha
Repubican hata kama hii ikimaanisha kufanya matakwa yao. Lakini
amesisitiza kuwa atafanya hivyo iwapo wajumbe hawa wataonesha nia ya
kutaka kumaliza kabisa mzozo huu wa bajeti.
Katika mkutano na waandishi wa habari
Rais Obama amesema kuwa majadiliano yanaweza akufanyika baina yake na
wajumbe wa republican, lakini kwanza bunge lote halina budi kuweka
mpango mkakatai wa kutafuta mbinu za haraka za kuweza kuendesha
serikali na kuitoa katika kifungo hiki cha muda kinachoumiza
wamarekani kwa sasa.
“Nitazungumza kuhusu lolote”
Alisema Rais Obama.
Hata hivyo Spika wa bunge hilo kutoka
chama cha Republican John Boehner, akiongelea swala hili jana,
alisema kuwa alipozungumz ana rais Obama kwa nji aya simu hakuon
alolote jipya. Na alikataa kuafikiana na matakw aya Rais Obama.
Boener alisema “Kama wajumbe wa
republican hawataki kuafikiana katika swala hili, basi atakaa
ilikuzungumza nasi” Lakini sidhani hivi ndivyo serikali yetu
inavyotakiwa kufanya kazi”
Wakati huohuo, John Boehner
anamatumaini kuwa hivi karibuni, wajumbe wakuu wakamati katika vyama
hivyo viwuili wataanza mazungumzo hivi karibuni.
Mjumbe huyu anayeiwakilisha Ohio
alisema “ Kutakuwa na makubaliano hivi karibuni” “hatutaweza
kutafuta suluhu la tatizo letu la sasa bila kufahamu na kutatua
tatizo lililotufanya tufikie hapa.