UGANDA NA MIAKA 51 YENYE VISA NA MISHIKEMISHIKE YA KISIASA.
0
Leo
Octoba 9, nchi ya Uganda inasherehekea miaka 51 ya uhuru wake
iliyounyakua kutoka kwa muingereza siku ya jumanne Oktoba 9 mwaka
1962.
Pamoja
na kuwa na marais wanane mpaka sasa, akiwemo huyu wasasa mwenye
rekodi ya kukaa kwa muda mrefu zaidi, Wananchi nchini Uganda
wanayoshauku kubwa ya kusherehekea miaka 51 ya uhuru wao.
Wakuu
wa nchi na serikali wamo kushudia maadhimisho haya lakini pia yumo
aliyewahi kuwa daktari wa Rais Museven ambaye pia ni hasimu wake
mkubwa wa kisiasa.
Besigye, alisema atashiriki maadhimisho hayo kwa kuwa lipewa kadi ya mualiko.
Hata hivyo hajawahi kushirki maadhimisho ya kitaifa kwa takriban
miaka 10 sasa.