WAZIRI MKUU LIBYA ATEKWA

0

Waziri mkuu wa Libya ametekwa nyara na watu wasiojulikana maajira ya asubuhi ya leo, ambapo watu hao walikuwa wamejihami kutoka hoteli iliyopo mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan
Taarifa kutoka Libya zinadai kuwa bwana Ali Zeidan ametekwa nyara na kupelekwa katika eneo lisilojukana, lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu tukio hilo. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda Zeidan amezuiliwa.

Mnamo siku ya Jumanne waziri mkuu Zeidan alitoa wito kwa Marekani na nchi za Magharibi kukomesha vitendo vya wapiganaji wenye itikadi kali nchini Libya. Kwenye mahojiano na shirika la habari la BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.

Waziri mkuu aliendelea kudai kuwa nchi yake inatumiwa kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya kanda hiyo.

Miaka miwili baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani Muammar Gaddafi, serikali la Libya imekuw aikifanya kila liwezekanalo kuwadhibiti makundi ya kijeshi, na majeshi ya kiislamu yanayoendelea kumiliki sehemu kadhaa za nchi hiyo.

Mapema wiki hii, Libya ilitaka maelezo kutoka kwa balozi wa Marekani nchini humo, kuhusiana na kukamatwa kwa mtuhuiw awa ugaidi wa kundi la Al-shabaab Anas al-Liby huko Tripoli.

Bw. Liby alikuwa miongoni mwa majina yaliyokuw ayakisakwa kwa udi na uvumba na Marekani kwa kutuhumi wkauhusika na mlipuko wa mabomu mwaka 1998, yaliyokumwa balozi za Marekani nchini Kenya na hapa Tanzania. Huyu alikamtwa jumamosi iliyopita.

Hata hivyo wadadisi wa mambo wanasema nimapema sana kuhusisha kutekwa kwa Waziri mkuu Zeidan na kutiwa mbaroni kwa Bw. Liby.

Mnamo mwezi wa nne mwaka huu waziri mkuu huyu aliwaasa wananchi wa Libya kuwa kitu kimoja na serikali yao iwapo wanataka amani ya kudmu. Alikemea sana vitendo vya uhalifu na hujuma kukithiri nchini humo.

0 comments: