MADAKTARI KENYA WAGOMA... WATAKA WAGONJWA WATAFUTE HUDUMA KWINGINE....

0
Umoja wa madakaktari na wauguzi nchini Kenya umeita mgomo wa kitaifa kwa wanataaluma hao kufuatia kushindwa kuafikiana na Serikali katika mazungumzo yaliyopangwa.

Katibu wa Chama cha Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno, Sultani Matendechere ametangaza kuwa mgomo huo utaanza usiku wa kuamkia leo katika hospitali zote za umma, hivyo wagonmjwa watafute njia mbadala za kupatiwa matibabu.



Watumishi hao wa afya wanapinga hatua ya serikali kuhamishia huduma za afya ikiwemo malipo ya mishahara yao kuwa chini ya kaunti, badala ya serikali kuu yenyewe. Kaunti ni mgawanyiko wa Nchi Mfano Kwa anzania tuna Mikoa, Lakini Kenya Zipo Kaunti nchini Nyingine yapo Majimbo.

Wafanyakazi hao katika sekta ya afya, wajumbe kutoka serikali za kaunti na serikali kuu walitumia takribani siku nzima jana katika kujadili matatizo yao ilikuepusha mgomo wa aina hii. Hata hivyo hawakufikia muafaka baada ya wafanyakazi hao kuapa kuingia katika mgomo iwapo matakwa yao hayatotiliwa maanani.

Kwa muda mrefu kwanzia kuanzishwa kwa mfumo wa kutoa madaraka kwa Kaunti hizi, Madaktari na wafanyakazi wengine katika sekta ya afya wamekataa sekta hiyo kuwa chini ya Majimbo yaani Kaunti badala yake wanataka sekta hiyo iendelee kuwa chini ya serikali kuu.

Watu wengi nchini Kenya wamekuwa wakipinga mfumo huu wenyewe wakiuita Devolution kwa sababu mbalimbali. Katika mfumo huu itakuwa kwamba Kaunti hizi ndizo zinzowalipa na kuendesha shughuli zoote za sekta. Kwa maneno mengine Uwezo wa kaunti kifedha ndiyo utakaoamua ni kwa jinsi gani sekta inaendeshwa. Madaktari wanahofu kuwa, Iwapo Kaunti kama ya Nairobi ndiyo yenye kipato zaidi na nyingine siyo, basi hii italipa wafanyakazi wake vizuri zaidi ya nyingine. Usawa, umakini utapotea katika sekta.

Mwenyekiti wa Asasi ya Wauguzi ya Kenya Bw. Nyaim Opot amesema kuwa mambo yahusuyo mafunzo, na taaluma nyeti hayapaswi kuwekwa chini ya Kaunti. Ni mambho yakushughulikiwa na serikali kuu. Hata hivyo awali asasi hii ilitoa muda wa wiki mbili wa kurekebishiwa madai yao vinginevyo wataingia katika mgomo na wiki hizo mbili ziliisha jana. Hivyo leo Wauguzi katika hospitali za umma wapo katika mgomo.

Tukumbuke kuwa, Ni kipindi kifupi kimepita tangu ipitishwe kura ya maoni kwa wananchi wa Kenya ya kuona ni wangapi wanaafiki Mfumo huu wa uendeshwaji wa shughuli. Katika kura hiyo, Mfumo huu wa kuzipa Kaunti madaraka ulipitishwa. Unaweza kushangaa iweje sasa kuwepo malalamiko ya aina hii? Tutafakari Waafrika Kura zetu ni za kushinikizwa? Au humaanisha yaleeeee tunayoyataka?

0 comments: