WAANDISHI KENYA WAANDAMANA KWA AMANI...

0

Waandishi wa habari nchini Kenya leo wameandamana kwa amani katika maeneo mbalimbali nchini humo kuonyesha kukerwa na muswada wa sheria unaokandamiza uhuru wa vyombo vya habari.

Wakati waandishi wakiandamana bunge la Kenya mchana wa leo linmekutana kufanya mabadiliko katika baadhi ya vipengele vya muswada huo uliopigiwa kelele mno na wadau wa habari.

Wajumbe wa kamati ya bunge wamekubali kupunguza faini kwa mwandishi atakaekiuka maadili kutoka shilingi laki tano za Kenya hadi shilingi laki moja, ambapo faini ya shs milioni 20 kwa chombo cha habari, pia itapunguzwa.

0 comments: