NDEGE KUTUMIKA KWA HOME DELIVERY.....upo apooo????

0

Amazon, shirika la kimataifa la biashara za rejareja hasa katika mtandao, linafanya majaribio yakuweza kutumia ndege zisizohitaji rubani kwa ajili ya kufikisha mizigo kwa wateja wao kwa haraka, usalama na urahisi zaidi.

Aina hii ya ndege ziitwazo Drones, zipo za ain nyingi lakini zinaangukia makundi makubwa mawili yaani zile zinazotumiw akwaajili ya uchunguzi fulani au zinazobeba mabomu ya milipuko. Ndege hizi huendeshwa na Rubani kutoka ardhini au zinaweza kuwa katika mfumo maalumu wakufuata programu zitakazo undiwa.


Mkurugenzi mkuu wa shirkia hili la kibiashara al Amazo Bw. Jeff Bezos says, ameweka wazi mpango wao huo akisema kuwa aina hii ya drone watakayotumia ijulikanayo kama Octocopters, inaweza kusambaza mizigo kwawateja yenye uzito, mpaka wa Kilogramu 2.3 ndani ya dakika 30baada ya wao kutoa oda.

Hata hivyo alidai kuwa inaweza kuchukua mpaka miaka mitano kwa huduma hii kuanza kutumiwa rasmi. Hata hivyo kitengo maalumu cha Anga nchini Marekani bado hakijapituisha matumizi ya ndege hiyo ijilikanayo kama Drone aina ya Octocopters. Bw. Bezos alipoulizwa kuhusu mchakato huo na inawezekana ni wakusadikika, alidai kuwa “Hii inawez akuonekana au kuchukulia kama jambo la kisayansi la kusadikika, lakini siyo. Ni kitu kinachowezekana."

Bosi huyu alisema hii itasaidi kusambaza takribani asilimia 86 ya bidhaa zote wanazosambaza kwa wateja wao. Haya sasa Bongo...Home delivery yenyewe..ni Tatizo Yaani kuletewa bidhaa nyumbani, bado tunaona ni gharama au ni Starehe Luxury, lakini wenzetu wamekwisha fikia kufikiria Drone delivery...Tutafika kweli????

Huduma hii ijulikanayo kama Prime Air, imeshambuliw avikali na wadadisi wa mambo wanaodai kuwa, kwa mwenendo wa uchumi kwa sasa. Sio rahisi sana kwa watu kuipokea vizuri huduma hii kwani wengi wangepend akuichunguz abidhaa, kuafikiana bei pungufu ndipo kuinunua. Na pi aitakua gharama zaidi kuendesha huduma hii hivyo haitakua na faida ya kutosha kwa kampuni. Hata hivyo Kampuni hii imetupilia mbali maoni hayo na kudai kuw aimekwishajipanga. Na kwamba inaweza kuanza kufanya kazi baada ya miaka mitano.

0 comments: