MAMA MWENYE WATOTO 10, AMLILIA MWANAE ALIYEMUACHIA RAFIKI.
Sasha Ruseva Mwanamke huyu Mbulgaria kutoka roma mwenye watoto 10 amejitokeza na kudai kuwa Mtoto
aliyepotea huko Ugiriki ni wa kwake na kwamba alimuacha huko kipindi cha
nyuma kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kulipia stakabadhi alizokuwa
anahitaji ili kusafiri.
Polisi wanaamini wataujua ukweli baada ya vipimo vya vinasaba. (DNA)
Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 35 anayetuhumiwa kuwa na tabia ya kuuza watoto ameapa kuwa hakuwahi kumuuza Maria na kwamba anamtaka sasa.
Hata hivyo imegundulika kuwa mwanamke mwingine aliyetumia jina lake amewahi kufungwa mara mbili huko ugiriki kwa kuuza watoto.