WANAFUNZI WAZIDI KUJIHUSISHA NA ULEVI BONGO:UTAFITI

0
Utafiti uliofanywa na mtandao wa kupambana na ulevi nchini Tanzania—TAANET umebaini kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo nchini Tanzania wamekuwa wakijihusisha na ulevi. 

 Katibu uenezi wa mtandao huo Bw. Mathias Kimiro amesema hayo katika mahojiano na East Africa Radio jijini Dar es Salaam leo ambapo amewataka vijana kuacha kunywa pombe kutokana na kinywaji hicho kuwa na madhara makubwa kiafya.



Kwa mujibu wa Kimiro, upatikanaji wa pombe tena ikiwa kwenye vifungashio vinavyobebeka kiurahisi maarufu kama viroba imetajwa kuwa moja ya sababu zinazochangia vitendo vya ulevi kwa vijana hususani wanafunzi

0 comments: