ALIYEKUWA NYOTA WA TAMTHILIA YA Isidingo LESEGO MOTSEPE “Letti Matabane" AFARIKI

0
Muigizaji mahiri Lesego Motsepe aliyejulikana zaidi kama “Letti Matabane” kwasababu ya uhusika wake katika Tamthilia maarufu Afrika kutoka Afrika Kusini Isidingo amefariki dunia akiw ana umri wa miaka 39.

Mwanadada huyu aliyekuwa Mhamasishaji na balozi wa UKIMWI alifariki JUmatatu ya Tarehe 20 mwezi huu.

Kwa mujibu wa wanafamilia alikutwa

amefariki nyumbani kwake huko Randburg, Afrika ya Kusini na kaka yake Moemise,ambapo uchunguzi wa madaktari nao ulionyesha hivyo.

Letti aligundulika kuwa aliathirika na virusi vya Ukimwi  kwanzia mwaka 2008. Ameacha Wazazi ndugu na marafiki.

 May her soul rest in peace, Amen.

0 comments: