SUDAN KUSINI BADO SANAAAA???? FAHAMU KWA KINA KINACHOENDELEA

0
Serikali ya Sudan kusini na waasi jana walisaini makubaliano ya kisitisha mapigano na ghasia zilizoharibu kabisa mandhari ya nchi hiyo kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya maelfu ya askari na wananchi..

Makubaliano hayo ya Amani, ni ya kwanza yenye tija tangu kuanza kwa mapigano nchini humo mwaka jana mwezi Desemba tarehe 15. Hata hivyo maswali kadhaa yalizuka iwapo watu wote wanaohusika na ghasia hizo watakubali kusitisha na itachukua mda gani hasa kwa wote kuacha kabisa mapigano.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini kanali Philip Aguer alionya kuwa vijana wadogo wanaoshirikiana na aliyekuw amakamu wa Riek Machar katik akundi lijulikanalo kama “Whiet Army” huenda wasikubali kusitisha mapigano. Alisema watoto hawa ni wadogo, wanashinikizwa na makundi hivyo hawana kabisa nidamu ya kijeshi.

Rais wa Marekani Barack Obama alipokea taarifa hizi kwa furaha na kuiita hatua moja muhimu na yenye changamoto nyingi ya kufikia amani ya kudumu.

Katika taarifamaalum Rais Obama amewataka viongozi wa Sudan Kusini kutekeleza makubaliano hayo yaliafikiwa na kuanz amazungumzo ya kisiasa ilikumaliza kabisa uhasama.

Alisema kuwa ni muhimu kwa mateka wote walioshikiliwa kuhudhuria mazunguzmo hayo ya kisiasa.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilipongeza hatua iliyofikiwa huku likitaka utekelezwaji wa haraka wa mafikiano yaliyofikiwa. Mazungumzo yanaendelea tena hii leo, Upande wa waasi unaongozwa na aliyekuwa makamu wa Rasi Riek Machar ukitaka kuachiwa kwa mateka 11 waliokuwa viongozi wa juu waserikali ambao Rais Kiir anasema hawanabudi kupitia mikononi mwa sheria.

Mradi maalum wa Marekani ujulikanao kama “The Enough Project” unaofanyia kazi maswala mbalimbali ya Afrika ya kati umesema wazi , kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo jana ni hatua moja tu. Bado hakuna uhakika wowote iwapo mapigano yatasitishwa, kwani hakuna anayefahamu nani atasalimisha silaha na nani hata fanya hivyo.

Mwanzilishi wa mradi huo Bw. John Prendergast amesema kuwa ipo haja ya kutafuta suluhu ya chimbuko au mizizi ya ghasia hizo na siyo kumaliza tu ghasia zilizopo kwa sasa.


Ijulikane kwamba, Hata kama waasi na serikali kwa ujumla wakikubali kuweka silaha chini na kuja katika meza ya mazungumzo, bado hatuwezi kuwa na Amani na utuluvu endelevi nchini Sudan kusini kama hakutafanyika mazungunzo ya kitaifa na kiserikali ya kujadili mfumo mzima wa utawala na sekta ya ulinzi na kuwepo uwazi wa marejesho na uwajibikaji katika sekta zote za serikali.






0 comments: