OBAMA AANGUKA KIUWEZO: FORBES

0
Vladimir Putin Raqis wa Urusi
Kuna msemo usemao kuwa wa kwanza si kazi.. Kazi kubaki wakwanza. Hili limemsibu Rais Barack Obama wa Marekani baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kutajwa kuwa mtu mwenye nguvu na ushawishi zaidi duniani kupitia jarida la Marekani la Forbes.

Putin amempiku Rais Barack Obama ambaye kwa sasa anashikilia nafasi ya pili katika orodha hiyo.

Habari kutokana na Jarida hilo zinaeleza kuwa Obama amekumbwa na anguko hili mapemo isivyo tarajiwa huku Putin akionesha uwezo wake mkubwa wa kukabiliana na mambo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa miaka mitatu ambapo Rais Obama ameangushwa kufikia nafasi ya pili katika Orodha ambayo hutolewa na Jarida hili la Forbes.

Barack Obama Rais wa Marekani
Hali hii imehusishwa na mshikemshike kati ya Marekani na Urusi katika Vita nchini Syria.

Rais Putin ambaye amekuwa akizitawala siasa za Urusi kwa muda wa miaka 12 sasa, alichaguliwa tena kama Rais wa nchi hiyo Mwaka jana mwezi machi.


Wakati huohuo, Rais Obama ameonekana kujeruhiwa kwa kufungwa kwa shughuli za kiserikali kwa muda wa siku 16 iliyosababishwa na misukosuko ya Bajeti nchini humo.

Swala lingine ni kuhusiana na Urusi kumpa ufadhili aliyekuwa Usalama wa Taifa wa Marekani Edward Snowden baada ya Marekani kumsaka kwa udi na Uvumba mnamo Agosti mwaka huu.

Barack Obama Rais wa Marekani
Mwezi mmoja baadae Putin alikuja na njia nyingine ya kukabiliana na Vita nchini Syri abadala ya ile ya Obama ya kupigana kivita. Na mawazo haya ya Putin yalifanyiwa kazi kuzidi kumuweka Putin juu zaidi. Imeelezwa kuwa mtu yoyote aliyetizama makubaliano haya yaliyofanywa kwa ajili ya Syria anaweza kukubaliana na mabadiliko haya katika jarida la Forbes.

Katika orodha hii ya watu wenye nguvu zaidi na ushawishi duniani yupo Rasi wa Uchina Xi Jinping katika nafasi ya tatu, Papa Francis 4, Angela Merkel kansela wa Ujerumani 5 huyu ni mmoja wa wanawake wawili walioingia 20 bora, Bill Gates katika nafasi 6, Ben Bernanke, gavana wa benki ya Marekani nafasi ambayo mwezi januari itachuliwa ma Bi Janeth ellen. Nafasiya 8 yupo Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz Al Saud, nafsi ya 9 rais wa benki kuu ya Ulaya Mario Draghi, na 10 mkurugenzi mkuu Wal-Mart Michael Duke.
Rais wa Uchina Xi Jinping

Nafasi ya 11 ni waziri mkuu wa Uingereza David Cameron is 11th most powerful, in the magazine's opinion - well ahead of his French counterpart but well behind American philanthropist Bill Gates.

Papa Francis wa 1.
Mwanamke mwingine kwenye list katika 20 bora ni Dilam Roseff rais huyu wa Brazil. Mwanamke mwingine Christine Largade wa IMF shirika la fedha duniani ameshika nafasi ya 35.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel




Na Kutoka Afrika Yupo Tajiri huyu ambaye opia amewekeza katika kiwanda cha Cementi Nchini Bw. Aliko Dangote akishikilia nafasi ya 64.


0 comments: