PAKA ATISHA POLISI KWA SIMUU...IONE HII...
0
Mapolisi katika eneo moja jijini
London, nchini Uingereza walishtushwa na kwenda mara moja eneo la
tukio baada ya simu ya hatari kupigwa bila ya kuwa na mzungumzaji
yoyote kwa upande wa aliyepiga.
Mapolisi hawa walipokimbia wakidhani
huenda aliyekumbwa na tatizo hilo yupo katika hali mbaya, wakiwa kwa
nje ya nyumba hiyo walisikia kelele za kuparuana, ndipo walipovunja
mlango wa nyumba hiyo na kushangazwa kumkuta paka aliyejulikana kwa
jina la Bruce akicheza na paka mwenzake katika gorofa hiyo
aliyejulikana kwa jina la Audrey.
Paka huyu alikuwa nyumbani, walezi wake
walipokwenda kazini na huenda alikua akitafuta kujaliwa kidogo yaan
“he was seeking attention”.
Hata hivyo Poilisi waliwataka
wamiliki wa Paka hao kueleza kilichotokea. Ambapo ilielezwa kuwa Paka
wake hukimbilia simu inapoita na anapenda kuchezea vibonyezo vya simu
hiyo. Mmiliki huyu amelazimika kutumia kiasi cha Paundi 100 Takriban
Shs. Laki 2 kw aajili ya kuurekebisha mlango wake... Upo apo...