MWENZA WA RAIS WA UFARANS ALAZWA KWA MAUMIVU YA MAPENZI???? NI MAPENZI TUU?

0
Valerie Trierweiler Francois Hollande Julie Gayet
Huko Ufaransa, Mpenzi wa Rais wa 24 wa Ufaransa Mwanamama wa kwanza nchini humo First Lady Valerie Trierweiler alipelekwa hospitali mapema mwishoni mwa wiki baada yakupata msongo wa mawazo kufuatia habario kuwa mume wake Rais Francois Hollande anamahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine.

Habari za mahusiano ya kimapenzi ya mumewe Francois Hollande na muigizaji zilimfanya ajisikie vibaya ghafla kwani alisikia habari hizo alhamisi iliyopita na mara tu akahitaji huduma ya daktari.

Mwanamama huyu mwenye umri wa miaka 48 


alikuwa hospitali mpaka hii leo inayosemekana ndiyo siku aliyotoka. Imesekana kuwa madaktari wamemtaka apumzike kwa wingi kwa siku kadhaa.Mama huyu alizidiwa na kulazwa hospitali siku ya ijumaa baada ya gazeti lililoandika habari hizo za mumewe kutoka.

Habari hizi zimekuja baada ya kura ya maoni nchini Ufaransa kuonyesha kuwa watu wengi wanataka Rais Francois aachane na mwana mama huyu. Zaidi ya asilimia 89 inataka Hollande aachane na mke wake huyu wa sasa. Wenyewe wanamuita quasi firstlady... tunawez akutafsiri kama first lady ambaye hajaandikwa kwa wino...kwani sio mke halali wa ndoa....

Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya ufaransa kwamba mke wa waziri mkuu anafukuzwa ikulu kabla ya muda wa uongozi wa mumewe kuisha. Pengine hiki ndicho kinamfanya mwanamama huyu aumwe.. Nafasi yake huenda ikachukuliwa na Muigizaji Julie Gayet, mwenye umri wa miaka a 41ambaye kwanzia mwaka uliopita amekuwa akidhaniwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa siri na Rais Francois Hollande.

Huyu mama analilia mapenzi au Hadhi yake kisiasa? Mwanamama huyu muandishi wa habari amekuwa akichukiwa sana na watu wa ufaransa japo hajawa maarufu sana nchini humo. Wananchi wanachukizwa zaidi na tabia yake yakufanya shughuli za First Lady wakati wanadhani yeye sio first lady...

Bi Trierweiler hajazungumza lolote kwanzia kuzuka kwa matatizo haya ijumaa,hata hivyo vyanzo vya habari karibu naye vinadai kuwa mama huyu amechoshwa na kudhalilishw asana kwa taarifa hizi. Ipo minong'ono inayiodai kuwa Rais Francois Hollande na mkewe wametengana kwa muda sasa na kwamba rais huyu anajipanga kuweka hadharani mahusiano yake na muigizaji Bi. JulieGayet.

Lakini ebu tutizame historia fupi ya mahusinao ya watu hawa ya kimapenzi... Wazungu wanasema “A relationship born in Betrayal will end in Ashes. Nakurudisha kidogo kwa stori ya muigizaji mashuhuru Elizabeth Taylor na aliyewahi kuwa mumewe maarufu Richard Burton...Japo wote hawa ni marehemu...

Ndoa ya Bi valerie ya kwanza kwa aliekuwa rafiki yake toka utotoni. Bw. Franck . Ndoa hii iliisha bila watoto. Kaolewa tena kwa mara ya pili kwa Denis Trierweiler, huko ndo alikochukua jina analotumia mpaka hivi sasa. Bw, Triewieler alikuwa mhariri katika gazeti maarufu la Match. Ndoa hii ilipata watoto watatu lakini ikaishia kwa talaka mwaka 2010. Talaka hii ilichukua miaka 3 kupatikana. Wakati huohuo Bi valerie na mahusiano ya kimapenzi na Francois Hollande.

Na mpaka leo Francois hajamuoa Valerie japo “wanaishi wote”.


Francois naye hakuwahi kuoa. Ukiachilia mbali madai ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi kila kukicha Mwenza wake wa kwanza ni bi Marie-Ségolène Royal ambaye alipata naye watoto 4 na kukaa naye takribani miaka 30 halafu kutangaza kuachana naye mwaka 2007.
Hata hivyo imeahidiwa kuwa taarifa kamili z amahusiano ya Francois holland enma tuhuma dhidi yake zitawekw awazi hapo kesho....Hatujui atatangaz akitu gani....

Inadaiwa kuwa Ufaransa ndiyo Tanga ya dunia..Je hii ndiyo sababu viongozi wake wajuu wanakutwa kwenye skendo za kimapenzi kila kukicha?

Tafadhali toa maoni yako....

0 comments: