MFAHAMU ZAIDI ARIEL SHARON..UNAJUA ALIOA MTU NA DADA YAKE?
0
Maelfu ya Waizraeli hapo jana walitoa
salamu zao za mwisho kwa mpendwa wao, kiongozi wao na aliyekuwa
waziri mkuu mstaafu Hayati Ariel Sharon hapo jana mwili wake
ulipowekwa nje ya jengo la bunge la Israel.
Mambo machache usiyafahamu kuhusu
Sharon. Ariel Sharon alizaliwa tarehe ya 26 mwezi
wa pili....1928. Alikuwa muisraeli na jenerali katika kikosi cha jeshi cha
nchi hiyo. Alitumikia Israel kama waziri mkuu wa 11 mpaka alipopatwa
na ugonjwa wa kiharusi uliomfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake
ipasavyo hivyo kuachia ngazi.
Alikuwa kamanda wa kikosi cha jeshi cha
Israeli kwanzia mwaka 1948.
Sharon ambaye alibatizwa jina la Man of Action
yaani mtu wa vitendo... amewahi kuwa mjane mara mbili. Alioa mke wake wa kwanza Margalit baada ya kuwa kiongozi wa kikosi ambaye walipata mtoto mmoja. Lakini Margalit alifariki dunia mwaka 1962 baada ya kupata ajali ya gari. Mtoto wao Gur alifariki mwaka 1967 baada ya kupigwa risasi na rafiki yake ambaye walikuwa wakicheza kama watoto kwa kutumia bunduki. Baadaye Ariel Sharon alimuoa mdogo wa mkewe wa Kwanza aliyeitwa Lily. Lily alikuwa mrembo sana. Walipata watoto wawili Omri and Gilad. Kwa bahati mbaya sana Lily naye alifariki dunia mwaka 2000 baada ya kupata ugonjwa wa saratani ya Mapafu.
Mamia walisikka wakisifia uwezo wake
mkubwa kijeshi na kwamba ni kati ya viongozi wachache waliojitoa kufa
na kupona kupigania nchi yao.
Ariel Sharon aliyefariki jumamosi
iliyopita baada ya kukaa katika hali ya kutojitambua yaani Coma kwa
takriban miaka nane amesababisha majonzi makubwa kupita kiasi nchini
Israel. Sharon ataagwa tena leo kiserikali na kuzikwa katika hafla
itakayoshuhudiwa na Viongozi wa kidumia kama Naibu Rais wa Marekani
Joe Biden na aliyekuw awaziri mkuu wa Uingereza Tony Blair.
Shughuli hii itaanzia Latrun
kutakapokuwa na mkutano wa viongozi wa kijeshi kabla ya mwili wa
Sharon kupelekwa shambani kwa Sharon Shikmim kwa ajili ya maziko.
Waziri mkuu Wa Israel wa sasa Benjamin Netanyahu amemuelezea Sharon
kwa kiongozi mzuri wa kiasiasa na kinara wa vita.
Hata hivyo watu wengine wametoa sifa
mbaya kwa Sharon hasa wakazi wa Ukanda wa Gaza na Palestina. Maamuzi
yaleyale yaliyomfanya Sharon kiongozi mtata wakati wa uongozi wake
mrefu kama kongozi wa Jeshi na mwanasiasa yalionekana tena pale tu
alipofariki.
Hii inajumuisha kuwa kwake waziri wa
Ulinzi manmo mwaka 1982 katika vita ya Lebanon. Wakati huo Sharon
alishikiliwa kama muhusika mkuu katika vifo vya maelfu ya watu waki
Palestina katika kambi za wakimbizi za Sabra Shatila. Alilazimishwa
kujiuzulu.
Aliwahi kusababisha adha kubwa pale
alipowaamuru waisraeli wajenge katika ardhi iliyosemekana ni ya wa
Palestina na baadae kugeuka ghafla na kuwarudishia wapalestina ardhi
yao kwa mara ya kwanza katika miongo minne. Rais wa Israel Shimon
Peres alitoa hotuba kwa ajili ya Sharon akimuita rafiki Arik Sharon
jina ambalo ni la utani kwa Sharon. Alimtaja kama mtu aliyetukuka
aliyewapenda watu wake an watu wake wakampenda zaidi.
Tunasema Bwana ametoa na bwana ametwaa
jina lake liimidiwe.
Watu mashuhuri na vinara wa nchi zao
wanapofariki, kunakuwa na hali za kufana katika nchi tofauti
tofauti...Je unafahamu zi zipi hizo...Tafadhali toa maoni yako...