UTI WA MGONGO ILIOPINDA WAGEUKA LULU
0
Mwanadada mmoja ajulikanaye kwa jina la
Leanne Roberts amegeuza hali ya ugonjwa au kilema alichokua nacho na
mgongo uliopinda kuwa fani yake baada ya kukataa matibabu yoyote ya
kioperesheni ya kuibadilisha hali yake.
Leanne mwenye umri wa miaka 18 alikua
na uti wa mgamgo wenye sura ya S uliokuwa ukimletea maumivu makali na
msongo wa mawazo, hata hivyo alichagua kufanya mazoezi kuliko tiba
nyingine yoyote.
Leanne Roberts |
Kwa sasa ni mwanamitindo anayetegemea
kufanya vizuri sana katika sekta hiyo kwani hiloo umbo lake
linamsaidia kuonekana anafaa sana kutokana na muonekano wake.
Hii inatukumbusha kuwa Tatizo lako
linaweza kuwa faraja yako.