FARASI AFANYWA MSIMAMIZI HARUSINI... AJABU NA KWELI...
0
MAHARUSI, MATRON NA PATRON WAO....LOLEST... |
Maharusi wapya walikuwa washitakiwe
kufuatia makosa ya kumtembeza farasi bila ruhusa maalum, baada ya
Bibi harusi kuamua kumuweka farasi huyo kama mmoja wa wasimamizi
wake. Mwanadada Alex Wells, mwenye umri wa miaka 28, alifanya uamizi
huo alipokuw akifanya mipango ya harusi yake huko Nottinghamshire,
Uingereza ambapo hata mume wake aliafikiana naye.
Farasi huyu aliyejulikana kwa jina la
Toffee, mwenye umri wa miaka 17 inasemekana pia kwa namna moja au
nyingine ndiye aliyeruhusu harusi hiyo kufanyika kwani ni rafiki wa
karibu sana wa Bi Harusi. Mume wa Alex, Graham Sales alikiri
kukubaliana na hali hiyo kwani hata kwenye maisha ya kawaida ni kama
anashindana na farasi huyo ili kupata muda na mkewe.
Farsi huyu alikuwa na wakati mzuri
wakati wa harusi hiyo kwani aliweza kushiriki katika kupiga picha za
pamoja na mambo mengine.