WANAWAKE WAKANGANYWA NA SIASA ZA KENYA....ZAMA HUMU

0
Nancy Baraza

ILIKUA NANCY BARAZA, IKAJA KUWA RACHEL SHEBESH, AKAFUATA GLADYS BOSS SHOLLEI NA SASA NI CHARITY NGILU...

Watajwa ni wanawake waliokuwa na ushawishi mkubwa au wenye ushawishi mkubwa sana nchini Kenya. Ni wanawake ambao waliingia kwenye skendal mbalimbali zilizowafanmya waachane na wadhifa wao au siasa kwa ujumla.

Tumewahi kusikia kuhusu yaliyomkumba Nancy Baraza Mwanamama aliyekuwa Naibu Jaji mkuu wa Kenya aliyeingia matatani baada ya kumfinya Pua na kumtishia maisha mlinzi katika soko moja kubwa nchini kenya iliyompelekea kufutwa kazi mapema mwaka 2012.

Rachel Shebesh

Baada ya mwaka mmoja ikafuata Rachel Sahebesh, Huyu anawakilisha wanawake wa Nairobi katika Bunge la Kenya. Achilia mbali skendo ya kwa na mahusiano ya kimapenzi na Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi almaarufu, MikeSonko, Shebesh amewahi kunaswa kibao na Gavana wa Nairobi Evance Kidero, hii kidogo ilimchafulia shebesh na kumuweka katika hali isiyokuwa nzuri kiasi. Lakini zaidi ya kuandikwa na Magazeti na kukataa kuwa hakumpiga kibao wakati picha za video zilionesha hilo, Evance Kidero hakuchukuliwa hatua zozote kali za kisheria.

Rachel Shebesh akiwa na Mike Sonko
Gladys Boss Shollei
Ikafuata Gladys Boss Shollei binafsi navutiwa sana na Mama huyu. Achilia mbali uwezo wake kiakili, Mama wa Familia, pia ni mrembo sana. Gladys Shollei alikua msajili katika mahakama ya Kenya kabla ya kufutwa kazi yake baada ya kutuhumiwa kusababisha upotevu wa mabilioni ya Sh. Kesi ambayo amekanusha madai hayo na kesi imeanza kusikilizwa wiki hii.

Gladys Boss Shollei
Kabla hili la kwake halijakaa vizuri, Sasa Bunge la Kenya limeitisha Mswada ukiongozwa na Wabunge wa Muungano wa Cord wakitaka mama huyu afutwe kazi kutokana na tuhuma za ukikukwaji mkubwa wa katiba ya Kenya katika uendeshwaji wa wizara yake. Wabunge nchini Kenya jana wamekiweka hatiani kibarua cha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Charity Ngilu, kutokana kuridhika kuwepo tuhuma za rushwa dhidi yake. Wabunge wamemtaka Waziri Ngilu kujiuzulu, na iwapo hatofanya hivyo wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kumfukuza la sivyo, wataanzisha mchakato wa kumg'oa Ngilu madarakani.

Kukubalika kwa ripoti ya rushwa inayomtia hatiani Ngilu, kunafungua milango kwa wabunge kuandaa rasimu ya kutaka waziri huyo afukuzwe kazi.
Charity Ngilu
Charity Ngilu ambaye anazungunziwa ndivyo sivyo na watafiti wa maswalal ya siasa, pia amewahi kuandamwa na kesi ya Rushwa katika wizara ya Maji aliyoitumikia katika serikali iliyopita tuhuma ambazo zilisambaratishwa kwa njia za panya. Wengine wamedirikiki kumuita (political Parasite)

Charity Ngilu
Ngilu aliyezaliwa mwaka 1952, alikuwa mwanamke wa kwanza kuliingia bunge la Kenya mwaka 1992 baada ya chaguzi za vyama vingi nchini Humo, na kuwahi kuwa kati ya wanawake wawili wa Kanwza kuwahi kujaribu kugombea kiti cha Urais Nchini humo mnamo mwaka 1997. Mwanamke mwenmzake waliogombea nafasi hiyo alikuwa ni Marehem Wangari Maathai mwanaharakati huyu wa Mazingira.

Marehemu Prof. Wangari Maathai
Swali linakuja Je! Hizi ni jitihada za kung'oa kina mama wanaoshikilia nafasi muhimu katika siasa za Kenya? HATA HIVYO IKUMBUKWE KWAMBA KINA MAMA HAWA WAMEKUWA WAKISHTUIMIWA KWA SHUTUMA ZENYE USHAHIDI....

Huenda kuna picha fulani tunapata kuhusiana na Mwenedno wa Siasa za nchini Kenya.... Toa maoni yako sasa...



0 comments: