UAMUZI WA KENYA KUFUNGAMANA NA TANZNAIA UNAASHIRIA NINI?????
0
Kenya
imekuwa nchi ya kwanza katika jumuiya ya Afrika Mashariki kwa
kuipongeza Tanzania kwa hatua yake ya kutangaza bayana kwamba haiko
tayari kutoka katika jumuiya hiyo kama ilivyokuwa ikidhaniwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Waziri wa mambo ya nchi
za Nje wa Kenya Amina Mohamedi amesema Kenya inaiunga mkono hotuba ya
Rais Jakaya Kikwete kuhusu uamuzi wake wa kutojitoa katika jumuiya ya
Afrika Mashariki huku akisisitiza kuwa bila ya Tanzania hakuna Afrika
Mashariki.
Kwa
upande wake waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa
kimataifa nchini Tanzania Benard Membe amesema masuala ya ardhi
katika jumuiya ya Afrika Mashariki ni kila nchi katika jumuiya hiyo
itumie ardhi yake kwa matakwa husika.
Je nchi za Uganda na Rwanda zilificha siri gani???
Once a Witch, Always a Wizard...