FAHAMU HISTORIA, NA MUSTAKABALI WA WAKIMBIZI WA SOMALIA HAPA....

0
Zaidi ya wakimbizi 500,000 wasomali wanaoishi nchini Kenya, wanatarajiwa kurejeshwa makwao Somalia, baada ya shirika la kuwahudumia wakimbizi hao la UN kutia saini mkataba na Kenya pamoja na Somalia kuhusu kuwarejesha nyumbani wakimbizi hao.

Kenya na Somalia zimesaini mikataba ya makubaliano ya kuruhusu kurejeshwa kwa wakimbizi hao nchini Somalia. Makubaliano hayo yamesainiwa jana na Waziri wa mambo ya nje wa nchini Kenya, Amina Mohamed, pamoja na naibu waziri mkuu wa Somalia pamoja na shirika la umopja wa mataifa la wakimbizi UNHCR. Naibu Rais wa Kenya William Ruto aliyeshuihudia makubalino hayo amesema kuwa hii inaweka misingi ya kuanzishwa kwa kamisheni maalum itakayoshughulikia kuhama huko kwa wakimbizi kwa hiari ikiw ani baada ya miaka 20 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wasomali hao watarejeshwa kwa hiari nchini Mwao katika kipindi cha miaka mitatu inayokuja. Wasomali wamekuwa wakitafuta hifadhi nchini Kenya kutokana na vita na umasikini nchini Somalia. Kambi mbili ambako wakimbizi hao wanaishi, Dadaab na Kakuma zinafanana na miji mikubwa kwa ajili ya idadi kubwa ya wakimbizi hao.

Baadhi ya wakimbizi pia wanaishi katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi ambao unajulikana kama Somalia ndogo kutokana na idadi kubwa ya wasomali wanaoishi mtaani humo. Wakimbizi wengi kutoka Somalia walitoroka kutokana na vita, baada ya serikali kuporomoka mwaka 1991. Wengi wao walizaliwa kambini na hawajawai kamwe kwenda Somalia. Serikali za Kenya na Somalia pamoja na UN zimeanzisha rasmi mpango wa kuanza maisha mapya nchini Somalia na kushiriki katika mpango wa kujenga upya nchi yao.

Naibu waziri mkuu wa Somalia Fowsia Yusuf Adam, alisema Serikali inajiandaa kuwapokea raia wake waliokuwa wanaishi ukimbizini. Umoja wa Mataifa umesema kuwa makubaliano ya kuwarejesha wakimbizi Somalia ni wito kwa jamii ya kimataifa kujitolea kutafuta suluhu la kudumu kwa mzozo ambao umeendelea kwa miaka mingi bila kikomo. Hata hivyo changamoto ni kuwa mkataba huo unawataka wakimbizi kurejea kwa hiari ingawa wengi wanaona Somalia bado ni mahala pasipo salama na hivyo itakuwa vigumu kwao kurejea. Lakini Je Nchi ya Somali ni salama kwa wakimbizi hawa....

Somali ni nchi iliyopo katika pembe ya Africa. Imepakana na Ethiopia upande wa Magharibi na Djibouti upande wa kaskazini Magharibi, bahari ya Hindi ipi mashariki mwa Somalia.Hali yake ya ardhi inajumuisha zaidi Milima midogo midoo n maeneo tambarare. Nchi ya Somali inajumla ya watu wapatao Mill. 10. Kufuatia vita vya wenywe kwa wenyewe mnamo mwaka 1991 Wasomali wengi waliondoka nchini humo kama wakimbizi ambapo kufikia mwisho wa mwaka 2009, watu wapatao 678,000 waliwekwa chini ya usimamizi wa shirika la wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR. Hii ilikuw akundi kubw azaidi duniani kuwekw achini ya usimamizi wa aina hii ukifuatiwa na Iraq na Afghanistan. Kufuatia mapigano yaliyoibuka kusini mwa Somali Takriban watui wapatao 132,000 waliondoka mwaka 2009, na wengine wapatao 300,000 waliharibiwa makazi yao ndani ya somalia.




 Ikumbukwe kwamba kwanzia mwaka 1991 baada ya serikali ya aliyekuwa Rais wa Somalia Mohamed Siad Barre kuvunjika kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe, Somalia haikuw ana serikali kuu. Badala yake wananchi walitafuta mbinu mbadala za kutatua matatizo yao kw akuweka sheria za vijiji, Dini na kadhalika. Hata hivyo kufikia miaka ya 2000, serikali ya mpito iliundwa. Serikali hii, haikuwapendeza wengi hivyo kupelekea kuwepo kwa waasi waliounda vikundi vilivyoipinga serikali iliyokuwep madarakani. Vikundi vyenye misimamop mikali zaidi viliundwa kama vile Al shabaab.



Kufikia Mwaka jana mwezi wa nane. Serikali ya Somali iliweza kupokonya sehemu kubwa ya kusini mwa Somali iliokuwa ikishikiliwa na kundi hilo kwa usaidizi wa mataifa mengine makubwa. Hata hivyo Hivi sasa Somali imeweka mkakati maalum wa kuleta wanawake, wanaume na vijana wa nchini humo pamoja ilikuleta Amani nchini Humo. Hili Linaweza kuchukua muda kiasi, lakini kama tulivyozoea nchini Nyingi za kiafrika, Rasili mali ndiyo chanzo kikubwa cha mapigano ya wenywe kwa wenyewe. Je kuna Rasilimali yoyote yenye Thamani ya Maisha ya Mtu? Huenda Hasira, chuki na Ubinafsi umefanya waafrika wengi wakaweka hili pembeni.


0 comments: