TATTOO YAMUUNGANUSHA NA FAMILIA

0
Indian police commando, Ganesh Raghunath Dhangade (R), shows a tattoo to his family in Thane district on the outskirts of Mumbai on October 16, 2013.
Dhangade akiwa na mama yake kushoto na nduguze
Polisi mmoja katika jiji kubwa la India Mumbai ambaye alipotea katika stesheni ya reli miaka 24 iliyopita, sasa ameungana na familia yake kwasababu tu ya tattoo aliyokuwa nayo mkononi.

Mwanaume huyu ajulikanaye kwa jina la Ganesh Raghunath Dhangade alikuwa mwenye umri wa miaka 6 alitengana na wazazi wake. Baada ya kutengana huko, alilelewa katika vituo vya watoto yatima mpaka ukubwa wake alipoanza kuisaka famili yake.

Kilichokuwa kinasaidia katika msako huo ni Jina "Manda"ambalo mamaake aliliandika katika mkono wa Mtoto wake wa kulia. Katia pitapita zake alifika katika nyumba moja na kumuona mama mtu mzima ambaye  alipoiona Tattoo yake mkononi alipiga kelele za shangwe huku akitokwa na machozi.

Majirani nao walikuja kufurahi pamoja na mama huyu... Mtoto ake aliyepotea alirejea nyumbani.

0 comments: