WATU 9 WAHUSISHWA NA KUMVAMIA DKT MVUNGI.....
0
Idadi
ya watuhumiwa waliokamatwa kutokana na tukio la kumjeruhi vibaya
mjumbe wa tume ya marekebisho ya katiba Dk. Sengondo Mvungi
imeongezeka na kufikia watu tisa baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa
wengine watatu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa Mambo ya
Ndani ya nchi Dk. Emmanuel Nchimbi pamoja na Kamanda wa polisi kanda
maalum ya Dar es salaam kamishna Suleiman Kova wamesema watuhumiwa
hao watatu wamekamatwa na mapanga matano ambayo yanasadikiwa kutumika
kumjeruhi Dk. Mvungi.
Amesema
watuhumiwa hao pia wamekutwa na simu moja ya mkononi ambayo inadaiwa
kutumika katika mawasiliano kabla ya kufanya tukio hilo, na katika
mahojiano na watuhumiwa hao wamebaini kwamba bado kuna wengine ambao
watatakiwa kukamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.