UBAKAJI WAKITHIRI : RIPOTI
0
Takwimu
za jeshi la polisi nchini Tanzania zinaonyesha kuwa kati ya wasichana
kumi wenye umri wa chini ya miaka 18, watatu wamefanyiwa vitendo vya
ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa.
Akifungua
mafunzo ya namna ya kukabiliana na vitendo hivyo kwa maafisa wakuu wa
jeshi la polisi nchini Naibu kamishna wa jeshi la polisi nchini
Rashidi Ally amesema kwamba tatizo la ukatili wa kijinsia bado ni
kubwa na hivyo linahitaji ushirikiano wa pamoja na wananchi.
Amesema
jeshi hilo limekuwa likifanya kazi ya kuhakikisha wa;e wote
wanaohusika na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa katika mkono
wa sheria lakini hayo yote yanategemeana na taarifa kutoka kwa raia
wema pale wanapoona mtu anafanya vitendo hivyo.