MMILIKI WA "THE UGLIEST DOG" AOMBOLEZA KIFO CHAKE

0
Mbwa anayesadikiwa kuwa na sura mbaya zaidi ya mbwa wote duniani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 8 tu. Mbwa huyu ajulikanaye kwa jina la Elwood alijizulia umaarufu mkubwa baada ya kuonekana kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi. Mmiliki wake Karen Quigley alithibitisha kifo cha kiumbe huyo mwenye sura ya ajabu aliyewah kushinda tuzo mwaka 2007 amefariki dunia mwishoni mwa wiki.

Mmiliki huyu mwenye umri wa miaka 52ambaye alizongwa na machozi alipomzungumzia mbwa wake alisema amesikitishwa sana na kifo hicho kwani kilikuwa cha ghafla sana na alifia mikononi mwake. 

Mwanamke huyu alimnunua mbwa Elwood kutoka kwa mmiliki wake wazamani mnamo mwaka 2006 baada ya mmiliki huyo kutaka kumuua kwani alionekana kuwa na sura mbaya hivyo alishindwa kufanya biashara.


Baada ya Elwood kufanikiwa kushinda tuzo ya mbwa mwenye sura mbaya zaidi, alipata mamelfu ya mashabaiki waliokuwa wakimtumia picha na barua mara kwa mara. Umaarufu wake pia ulipelekea kuandikwa kitabu kilichoitwa ‘Everyone Loves Elwood’.





Yaani kila mtu anampenda Elwood.

0 comments: