Rais Jakaya Kikwete ameongoza watanzania kuadhimisha siku ya ulemavu.

0
Tanzania leo inaungana na nchi nyingine za Afrika Mashariki kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.


Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu nchini Tanzania Amon Anastaz maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Amesema kauli mbiu ya siku hiyo ni ondosha vizuizi fungua milango kwa ajili ya jamii jumuishi kwa wote.

0 comments: