HEKAHEKA ZAENDELEA KUKOKOA WACHIMBAJI AFRIKA KUSINI...

0
Waokoaji wa dharura nchini Afrika ya kusini hiyo jana walikuwa katika heka heka kutaka kuokoa wafanyakazi 9 wa mgodini ambao bado hawakuonekana katika mgodi uliokuwa ukiungua moto magharibi mwa jiji la Johannesburg.

Wamiliki wa mgodi huo, Harmony Gold walisema kuwa juhudi za kuokoa hao walioumizwa zilikuwa zikiyumbishwa na moshi mkali uliokuwa ukitoka baada ya kuporomoka kwa miamba. 9 kati ya wafanyakazi 17 ambao awali walikuwa wamekwama ndani ya mgodi huo bado ya wengine nane kuokolewa mapema hiyo jana.

Moto huo ulizuka umbali wa kilomita 1.7 chini ya ardhi katika mgodi wa Doorkop majira ya jioni ya juzi nainasemekana ilitokana na tetemeko la ardhi. Inasemekana tetemeko hilo lilisababisha hitilafi ya umeme katik amgodi huo kusababisha moto ambao mpaka wakati wa uokoaji ulikuwa ukiwaka.
Uongozi wa kampuni hiyo iliwaomba sana waokozi kufanya jitihada kumaliza shughuli hiyo kwani hata mirija ya hewa safi ilikwisha pata hitilafi.

Licha ya juhudi za kuhakikisha mazingira salama migodini,
bado ajali nyingi zinaendelea kutokea nyingine zikisababishwa na uzembe. Zaidi ya watu 120 waliuwawa mwaka 2010. Kutafuta wachimbaji madini waliozama ndani ya migodi imeendelea kuwa tatizo hata hivyo makampuni makubw ahutumia mifumo maalumu kuhakikisha wanabaki salama huko chini.

Tarifa zinadai kuwa, Wawekezaji walipoambiwa kuhusu hili hawakuonekana kuogopa au kushtushwa na taarifa hizo. Sekta ya madini ya dhahabu nchini Afrika kusini imezorota kiasi fulani kwa miaka 40 iliyopita, kutoka kuwa nafasi ya kwanza duniani kufikia ya sita


.
Afrika kusini ilizalisha takribani Kilo 167,235 za dhahabu mwaka 2012.

0 comments: