Hili Hapa Onyo La Nape Nnauye kwa Vijana Wanaotizamia Uanasiasa

0
Nape Nnaye
Katibu wa Nec Itikadi , Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ameonya vijana wanaingia kwenye siasa kwa kusaka Fedha kuwa sio hali halisi katika Siasa.

Nape Nnaye Prudence Gerald
Akiongea na www.prudencegerald.blogspot.com Nape amesema kuwa, siasa ni wito na utumishi. Akizungumzia historia yake binafsi ambayo anasema kuwa angetamani vijana wengi zaidi waifahamu, Nape amesema kuwa alipoanza siasa, alikuwa akilipwa kiasi cha Shilingi Elfu Themanini kwa takribani miaka nane (Japo hakua akitegemea fedha hizi kuendesjhea maisha yake ya kila siku. Baada ya hapo ndipo aliopata nyadhifa ya ukuu wa Wilaya na kuanza kula matunda ya Siasa ambayo vijana wengi wanatamani wayapate Haraka haraka.

Kwa upande wa katiba Mpya Katibu huyu wa Nec Itikadi , Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi amesema kuwa anamatumaini kila kitu kitakwenda sawa na watanzania wataipata katiba wanayoitaka.

Nape Nnauye na Prudence Gerald



0 comments: