Kesi ya Rwanda yenye UTATA, yasikilizwa Ufaransa
0
Miaka ishirini bada ya mauaji ya mauaji
ya Kimbari nchini Rwanda, (Genocide), nchi ya ufaransa sasa
imemfungulia mashtaka mtuhumiwa mmoja anayetuhumiwa kuhusika na
mauaji ya takriban watu laki 8.
Aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha kiintelijensia nchini Rwanda Bw. Pascal Simbikangwa amejisalimisha
mahakamani hapo hiyo jana katika kesi ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa
hamu, huku mashahidi wakisafirishwa kutoka Rwanda kwenda kutoa
ushahidi dhidi ya bwana huyo.
Bw. Pascal mwenye umri wa miaka 55,
aliyepatwa na ukilema kwanzia mwaka 1986, anatuhumiwa kuhusika sio
moja kwa moja na mauaji
ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Alikwisha pata
kifungo katika jela ya ufaransa iliyopo katika kisiwa cha Mayotte
mwaka 2008. hata hivyo wakili wa Bw. Pascal Simbikangwa anasema kuwa
mteja wake anakataa tuhuma hizo iwapo atakutwa na hatia basi
atatumikia kifungo cha Maisha Jela.
Kesi hii inasemekana ni ya utata kwani
hakuna mashahidi wa moja kwa moja.
Maujai haya ya kimbari yalihusisha
wanaharakati wa jamii ya wahutu waliolenga kuwauwa wale wa jamii ya
watutsi katika miezi mitatu ya mauji mnamo mwaka 1994. Hata hivyo
wale wahutu walioonekana kupingana na utaratibu waliathirika na
ghasia zilizosababisha kuangushw akwa ndege aliokuwamo Rais wa Rwanda
wa wakati huo Bw.Juvenal Habyarimana.
Bw. Simbikangwa Mtuhumiwa huyu aliachana na kazi za jeshi baada ya kupata ukilema hivyo kujiunga katika
kitengo cha Intelijensia.
Wengi wa ndugu jamaa na marafiki wa
walioathiriwa na mauaji hayo wamekuwa wakisubiri kwa hamu kusikilizwa
kwa kwesi hii, huku wengi wa washitaki wakisema hawataki kulipiza kisasi bali wanataka haki itendeke.
Nchi ya ufaransa imeshutumiwa kuwa
naugumu wa kuwatia hatiani watuhumiwa wa kesi hizi, ukilinganisha na
nchini nyingine kama Ubeljiji, ziliwatia watuhumiwa hatiani mara moja.
Mabadiliko ya kisheria mnamo mwaka
1996, uliipa uwezo Rwanda kupeleka wananchi wake watuhumiwa wa kesi
za mauaji haya kusikilizwa katika mahakama za Ufaransa. Ufaransa iliwahi kupigwa faini na mahakama ya ulaya ya haki za binadamu mnamo
mwaka 2004 kwa tabia hii ya kuchelewesha kutolewa kwa haki.
Wadadisi wanadai kuwa hii hutokea
kwasababu ya kukosa utayari wa kisiasa. Hata hivyo Rwanda iliwahi
kuvunja mahusiano yake na ufaransa mwaka 2006 yaliyorejea tena miaka
mitatu baadae.
Kesi hii ya Bwana Simbikangwa, ni hatua
muhimu katika kuendelea kuweka msingi imara wa daraja madhubuti baina ya nchini hizi mbili. Hukumu ya kesi hii inategemewa kutolewa
katikati ya mwezi machi mwaka huu.