UIGIZAJI UNAPOTEZA MUDA NA NGUVU..Asema Kala Jeremiah

0
Rapa Kala Jeremiah, ameweka wazi kuwa usanii wake yeye kiasili ulianzia katika uigizaji kabla ya kuhamia katika muziki, na kwa mtazamo wake yeye, sanaa ya Filamu hapa Bongo hailipi vizuri ukilinganisha na muda pamoja na nguvu ambazo waigizaji huwekeza katika kazi hiyo.

Kala amesema kuwa anapenda sana kuigiza na pengine baada ya atarudi kwa kasi katika fani hiyo, lakini kwa sasa haoni sababu ya kufanya hivyo kutokana na uchache wa malipo, hapa Kala anafunguka mwenyewe.

0 comments: