MADONNA APIGWA STOP JUMBA LA SINEMA

0
Madonna hajakatazwa kuigiza Sinema bali amepigwa stop kuingia katika majumba kadhaa ya Sinema huko Marekani kutokana na tabia yake ya kutuma ujumbe mfupi kila wakati.

Hivi karibuni yamemkuta haya katika uzinduzi wa filamu ya "12 Years a Slave" huko New York alipokuwa akiibonyeza bonyeza simu yake aina ya Blackberry.  Alipoguswa na mwanamke mwingine aliyekuwa katika jumba hilo, akimtaka aache kwani anawaharibia umakini wao, Madonna alijibu ni mambo ya kibiashara...siwezi kuacha... " enslaver"... Hili lilikera wengi na kumpelekea kuadhibiwa.





0 comments: