MWANDISHI UFUO SARO AJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI, MAMA YAKE AFARIKI PAPO HAPO

0
UFUO SARO.

Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufuo Saro amedaiwa kupigwa risasi ya tumbo na bega na kupelekea kumjeruhi vibaya,  huku mama yake mzazi akifariki papo hapo baada ya kupigwa risasi.
Habari zinasema kuwa, mwandishi huyo alihudhuria Kitchen party ya mfanyakazi mwenzake wa ITV ambapo alikaa huko mpaka usiku sana. Huku nyuma mume wake huyu mtarajiwa alirejea kutok akazinini huko Sudan ambapo alimkosa nyumbani. Alijaribu kumtafuta sana kwa simu bila mafanikio. Ufuo aliporudi wakaonana na huyu bwana. Lakini hakuridhishwa na maelezo aliokuwa akitoa Ufuo. Alfajiri walitaka kwenda huko kwa mzazi wa Ufuo kuyamaliza. hata hivyo habari za chini ya Carpet zindai kuwa Huyu Bwana aliona kama mama yake Ufuo anamtetea ndipo alipochukua uamuzi huo.

Hata hivyo kwa mujibu wa waandishi walioshuhudia gari waliyokuwa wakitumia, lilikuwa na vifaa vya kutatanisha. Yaani pengine bwana huyu alikwisha panga matukio haya yote.

Tukio hili lilitokea walipokuwa katika mazungumzo eneo la Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ndipo kijana huyo akadaiwa kuwafyatulia risasi na kisha kujiua kwa risasi. 

Hata huvyo Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi, mapema leo aliweza kumuona Ufuo Saro hospitalini na kusema kuwa hali yake inaendelea vizuri.

POLE SANA UFUO SARO. MUNGU AKUSAIDIE NA KUKUTIA NGUVU.


0 comments: