SERIKALI YA KENYA YATAKA WESTGATE MPYA
0
Baada ya uharibifu mkubwa uliotokana na kitendo cha Ugaidi kilichofanyika nchini Kenya Tarehe 21 ya Mwezi wa tisa mwaka huu na kuharibu kabisa jengo la kibiashra la Westgate, sasa serikali ya Kenya imesema inataka kulitengeneza upya.
Waziri
wa mambo ya Afrika mashariki, Biashara na utalii Phyllis Kandie
amesema leo kuwa wizara yake imeanza mipango ya marekebisho ya jengo hilo kufuatia shambulio la kigaidi mwezi uliopita.