TFDA, POLISI WAENDESHA OPERESHENI MAALUM YA MADAWA
0
Mamlaka
ya chakula na dawa nchini Tanzania kwa kushirikiana na
Jeshi
la polisi la shirikisho la kimataifa la Interpol imefanikiwa
kukamata
jumla ya dawa bandia za aina mbali mbali 273 zenye thamani ya
shilingi Milioni 49,634,733 katika operesheni maalum iliyopewa
jina la GIBOIA.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo,
ROBERT MANUMBA |
Mkurugenzi
wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini Tanzania DCI
Robert
Manumba amesema katika operesheni hiyo iliyoanza tarehe 1
hadi
3 ya mwezi huu walikagua maduka ya kuuzia dawa ya jumla na
reja
reja, waingizaji wa dawa nchini, pamoja na vituo vya afya na
maabara
binafsi.