HAS DEMOCRACY IN THAILAND FAILED OR IT IS JUST NOT THE SOLUTION...
0
Ghasia na maandamano ya upinzani nchini
Thailand, yamechangia kuchafua hali ya utulivu na amani katika chaguzi kuu zilizofanyika nchini humo hapo jana.
Ghasia hizi zilipeleea kusitishwa kwa
zoezi la kupiga kura katika sehemu za Bangkok na kusini mwa nchi
hiyo. Hata hivyo maafisa wamedai kuwa takriban asilimia 89 ya vituo
vyote vya kupigia kura vilifanya kazi kama kawaida.
Tume maalumu ya chaguzi ilisema kuwa
ghasia hizo ziliwaathirri karibia watu mill. 6. Waziri mkuu wa nchini hiyo mwana mama
Yingluck Shinawatra aliita chaguzi hizo akidhani zingemaliza ghasia za upinzani zilizoanza wii kadhaa zilizopita.
Japokuwa Chama chake kinakubalika sana
nchini humo, na kinategemewa kushinda., changamoto kadhaa za kisheria
na maelewano mabovu baina ya wanasiasa yanaweza kuleta mkanganyiko
fulani. Baada kutangazwa kwa hali ya hatari
nchini Thailand, maeneo kadhaa yamedhibitiwa huku kukiw an aulinzi wa
kutosha.
Maafisa wa usalma wamesema kuwa,
takriban askari 130,000 walitawanywa maeneo mbalimbali ya nchi hiyo
hapo jana na wengine 12,000 kuwepo katika mji mkuu wa Bangkok.
Chaguzi hizi zilikuwa na mambo kadhaa
yasiyo ya kawaida.
Tofauti na chaguzi za awali
zilizozoeleka kufanyika kwa amani, Chaguzi hizi zilifanyika katika ghasia zikidhaniwa kumaliza ghasia zilizopo. Hata hivyo kiongozi wa upinznaia Bw.
Suthep Thaugsuban amesema itakuwa ngumu kwa serikali kutangaza
matokeo kwani utata ni mwingi sana katika chaguzi hizi hasa
ukizingatia sio wote waliotaka kupiga kura hiyo walifanikiwa.
Maandamno ya upinzani yalianza mwaka
jana mwezi Novemba, baada ya serikali ya Thailand iliyopo chini ya
waziri mkuu bi Yingluck kutaka kupitisha sheria ya msamaha ambayo
ingemrudisha nchini Kaka yake Bw Thanksin ambaye amewahi kuwa waziri
mkuu nchini humo wakati alikuwa akiishi uhamishoni. Bw huyu alitoroka nchini alipokuwa na
kesi ya kujibu mwaka 2008 na inasemekana anaendesha nchi akiwa nje
kwa mgongo wa mdogo wake mwana mama Yingluck.
Japo kuwa chama cha mama huyu kina
wafuasi wengi, mkanganyiko wa vitambulisho vya kujiandiskisha kupiga
kura vinaweza kumfanya asipate wabunge wengi safari hii, hivyo kukosa
mamlaka ya kutosha juu ya Serikali. Chaguzi ndogo zinatarajiwa.
Wakati bi Yingliuck na chama chake
wakiwa na kesi nyingi za kujibu mahakamani, wafuasi wa mwana mama
huyu wanahofu, huenda
mahakama ikaingilia matokeo ya chaguzi hizi.
Chaguzi za jana zilikuwa na utofauti
mkubwa sana na zile zilizopita miaka mitatu iliyopita, ambapo Bi
Yingluck aliacha kazi yake nzuri aliokuw aakifanya kama mkurugenzi
katik akampuni nak uingi akatik asiasa na kusababisha kushind akw
akishindo kwa chama chake cha Puea Thai Party.