Apotelea Bahari ya Pacific miezi 16...Alikunywa mkojo kuishi...
0
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mzee
moja aliyesadikiwa kupotelea baharini kwa miezi kumi na sita, sasa
amerejea nchini kavu, kukiwa na maswali mengi ikiwa iliwezaji kuishi
katika mtumbwi wake mdogo kwa muda wote huo, huku kukikwa na hali
tete bahari ya Pasifiki?
Mwanaume huyu anayejiita Jose Salvador
Alvarenga alitokea katika visiwa vilivyojificha vya Marshall huko
Mexico akiwa na mtumbwi wake ulioharibika, akisema kuwa alikuwa
akiishi kwa kutegemea samaki na wanyama wengine wa bahari pamoja na
kunywa maji ya mvua na wakati mwingine mkojo wake mwenyewe. Alikuwa na kijana mwingine ambaye alifariki kwani alikataa kula ndege na
sasmaki wabichi na hakuweza kunywa mkojo wake.
Bado mamlaka nchini humo zinafanya
jitihada kufahamu ukweli wowote juu ya hadithi ya bwana Alvarenga.
Serikali ya Mexico imetoa tamko kuthibitisha kuwa Bw. Alvarenga ni
mwananchi wa El Salvador.
Familia ya Bwana huyu ilipotafutwa
ilikiri haijawasiliana naye kwa muda mrefu sana na walidhani pengine
alikwisha fariki. Bw. Alvarenga ana mtoto wa kike mweye umri wa miaka
12 ambaye hamkumbuki baba yake.
Hali tete iliyopo katika bahari ya
Pasifiki inafanya hadithi ya bwanahuyu kuonekana ni ya kusadikika.
Hata hivyo mawimbi yngeweza kuibeba boti hiyo kwa kilometa 42 kwa
siku kutoka Mexico mpaka visiwa vya Marshall. Hivyo kutokana na
wataalam hadithi yake inaweza kuwa ya kweli.