Bensouda Akalia Kuti Kavu ICC kesho...Zama Humu
0
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta |
Majaji katika mahakama ya kimataifa ya
makosa ya kihalifu ICC kesho watafanya maamuzi iwapo kesi ya Rais wa
nchini Kenya Uhuru Kenyatta itafutiliwa mbali au kuwapa mud azaidi
upande wa wachitaki kutafuta ushahidi zaidi.
Maamuzi hayo yatafanyika mkutano maalum
ambapo wanasheria wa Rais Kenyatta watafanya jitihada za kutaka
kumalizika kwa kesi hiyo, hata hivyo Rais Kenyatta hatahitajika
kusafiri kwenda The Hague kwa ajili ya mkutanio huo.
Wakati huohuo, upande wa mashtaka
unaoongozwa na mwana mama Fatou Bensouda utatafuta muda zaidi wa
kupata ushahidi mpya na mashahizi wengine, baada ya kuripotiw akuwa
mashahidi wengine walijiondoa katika kesi hiyo.
Bi. Fatou Bensouda |
Bi Bensouda anapinga kufutiliwa mbali
kwa kesi ya Bw. Kenyatta na ameituhumu serikali ya Kenya kwa kwa
kutoupa ushiriakiano upande wake katika uendeshwaji wa kesi hiyo.
Kesi ilipangwa kuanza kusikilizwa tena hiyo kesho.
Rais Uhuru Kenyatta |
Katika majibu yake Bi. Fatou Bensouda
aliwaomb amajaji kutupilia mbali ombi hilo. Alisema angehitaji kwanza
majaji hao waweke shauri lake lililolalamikia ushirikiano mbovu wa
serikali ya Kenya katika uendeshwaji wa kesi hio ambao ulikuwa
ukikiuka Mkataba wa Roma yaani ( The Rome statute)
Bi bensoud aalisistiza kuwa, kwa kuwa
Kenyatta ndiye Rais wa Kenya anauwezo wa kushinikiza lolote analotaka
lifanyike nchini humo. Mahojiiano ya mkutano huo wa kesho yanazidi
kuwa ya moto kwa kuzingatia matakwa yaliyopendekezwa na Umoja wa
Afrika, ulioiambia ICC, kuwa endapo watashindwa kufanya yale umoja
huo unayoyataka basi nchi za Afrika zitajitoa ICC kufikia tarehe 30
ya mwezi wa nne mwaka huu.
Katika barua hiyo iliyoandikwa Tarehe
29 mwezi wa kwanza AU imeainisha vitu kadhaa vinavyotakiwa
kushughulikiwa. Kama vileutaalamu udhihirike katika kutafuta
mashahidi na kufanya uchunguzi, na pia mahakam iache au kusitisha
kupokea fedha kutoka kw awahisani wanaowez kushinika mwenedno wa
kesi. AU imeitaka mahakam hii kutoa mpango mkakati watakao utumia
kurekebisha haya kufikia mwisho wa mwezi wa wanne
Kumbuka mvutano baina ya nchi
zilizoegema Ufaransa na zile za Uingereza unaweza ukawa na nguvu
katika mvutano huu wa ICC. Utambue Nchi za karibu na Ufaransa
(Francophone) countries sio wanachama wa ICC... Kesi karibu nane
zilizopo ICC ni za Waafrika..Lakini pia nchini kama
Marekani...Unafahamu kuwa yenyewe ilipitisha sheria ya kuwapa kinga
watu wake namahakama hiyo..
Unadhani Nchi za Afrika kuwa wanachama
au sio wanachama wa ICC kunaiongezea au kuipunguizia ICC kitu gani?
Mbona basi Umoja wa Afrika umetoa onyo la aina hii?