SIKU YA SARATANI DUNIANI...ONA TAHADHARI ILIYOTOLEWA
0
Shirika la Afya duniani WHO limeonya
kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa
saratani kote duniani. Shirika hilo limesema nusu ya maambukizi ya
saratani yanaweza kuzuiwa na kwamba juhudi mpya zinastahili kufanyika
ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupita kiasi, ulevi na uvutaji
sigara.
Watu milioni kumi na nne wanajulishwa
kuwa wanaugua saratani kila mwaka, lakini idadi hiyo inatarajiwa
kuongezeka na kufikia milioni ishirini na nne katika kipindi cha
miongo miwili ijayo.
Taasisi ya utafiti wa kimataifa kuhusu
ugonjwa wa saratani katika shirika la WHO lilionya kuwa gharama ya
matimabu inaongezeka kwa kiwango ambacho ni vigumu kumudu. Taasisi hiyo imesema serikali
zinahitajika kutekeleza sheria kali zaidi kuhusu matumizi ya pombe na
sukari kama vile kuongeza bei na kukataza matangazo ya kibiashara ya
bidhaa hizo.
Wakati huohuo, Wanasayansi wanaamini
kuwa unywaji mwingi wa pombe unaweza kuleta hisia zisizo za kawaida
mwilini ambazo zinaweza kuiweka ngozi katika hatari zaidi ya kupata
Saratani ya ngozi.
Kemikali ya Ethanol inapogeuzwa kuwa
“Acetaldehyde” baada ya ulaji wa chakula,kemikali hii yaweza
kuiwezesha ngozi kupenyeza miale hata ya jua (UV light).
Watafiti waliofanya ugunduzi huo, nchini Uingereza wanakubali kwamba kuna mambo mengine yanayochangia mtu kupata Saratani ya Ngozi.
Sarah Williams wa Utafiti wa Kansa,
Uingereza alisema ''Utafiti umeonyesha kuwa wagonjwa wanaougua
Melanoma huathirika kwa ajili ya kuota jua kwa muda mrefu,hili
linaweza kupunguzwa iwapo mtu atajikinga kutokana na jua kali.
Kulingana na utafiti wao uliochunguza mada 16 tofauti na kushirikisha
maelfu ya watu,unywaji wa chupa moja ya pombe moja au zaidi kila siku
huongeza uwezekano wa kupata Saratani ya ngozi kwa asilimia ishirini.