DOLA MILL. 54 ZAIBWA LIBYA KWA SILAHA
0
Shirika
la habari nchini Libya limeripoti kuwa watu wenye silaha wameiba
kiasi cha dola milioni 54 katika shambulio la basi dogo lililokuwa
limebeba fedha za nchi hiyo na za kigeni za benki kuu ya Libya.
Wanaume
hao kumi walilisimamisha basi hilo dogo wakati likiingia katika mji
wa Sirte kutoka Uwanja wa ndege ambapo fedha hizo zilisafirishwa
kilomita 500 kutoka mji mkuu wa Tripoli.
Serikali
ya Libya imekuwa ikifanya jitihada za kudhibiti uhalifu katika nchi
hiyo iliyojaa vikundi vya wapiganaji wenye silaha, wahalifu na
waislamu wenye msimamo mkali.