M23 SASA WAFIKA KIAMA
0
Mjumbe
maalum wa Umoja wa Mataifa katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya
Kongo ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa waasi wa
M23 ni kama wamedhibitiwa kabisa na si tishio tena.
Mjumbe
huyo Martin Kobler amesema waasi wa M23 wameng'olewa katika ngome yao
kuu ya Rutshuru na kwa sasa wamejikusanya wakiwa kundi dogo karibu na
mpaka wa Rwanda.
Ngome
hiyo ni ya tano kutwaliwa na vikosi vya serikali katika mapambano
yaliyodumu kwa wiki moja yaliyowasambaratisha waasi hao wa M23. Hata
hivyo waasi wamesema kuachia ngome zao hizo ni kwa muda tu.