Syria Yamaliza Mkutano wa Geneva..Bila Suluhu..Fahamu Zaidi
0
Pande mbili zinazozozana nchini Syria zinamaliza duru la kwanza la
mazungumzo ya amani hii leo, kukiwa hakuna mustakabali wowote
ulioafikiwa kumaliza ghasia zilizoenea nchini humo.
Serikali ya Syria pamoja na wawakilishi wa upinzani, wote wanatuhumiwa kuhusika katika ghasia na vita vya wenywe kwa wenyewe nchini humo japokuwa mazungumzo haya ya Geneva yaliegemea zaidi swala la Ugaidi.
Wakati makubaliano katika mazungumzo haya yangeonekana ni hatua muhimu ya kumaliza kabisa mgogoro wa Syria, mkutano huu unamalizika hii leo bila muafaka wowote.
Muwakilishi wa Umoja wa mataifa ambaye anasuluhisha pande hizo Bw. Lakhdar Brahimi, amesema kuwa wote wamekubaliana kuwa kunatatizo kubwa la ugaidi nchini Syria, japo hakuna upande wowote uliotoa suluhu ya nini kifanyike.
Pande hizo mbili zimeletwa pamoja mjini geneva ikiwa ni shinikizo kubw ala kidiplomasi ala kujaribu kumaliza vita ya wenywe kwa wenyewe nchini Syria iliyopoteza maisha ya zaidi ya watu 130,000 na kulazimu kupoteza makzi kwa mamilioni ya wananchi wa Syria.
Siku ya sita ya mazungumzo hayo hapo jana, ilianza vizuri kwani pande hizo mbili, zilianza kwa ukimya wa muda wakikumbuka waathirika wa ghasia za nchini Syria. Lakini katika hali ya kushangaza, umoja huu ulionekana sio umoja pale ambapo kila upande ulidai ndiyo uliokuwa ukitaka kuwakumbuka waathrika hawa.
Wawakilishi wa Serikali ya Rais Assad ulioudhuria mkutano huo, ulidai kuwa, swala la Assad kubaki kuwa rais sio la kuzngumziwa Geneva. Ni swala ambalo litabaki kama lilivyo.
Hata hivyo msuluhishi wa mgogoro huu Bw. Brahmi alisistiza kuwa ni muhimu kuweka serikali ya Mpito kwani haina maana kuzungumzia jinsi ya kuiongoza Syria wakati kuna ghasia. Ni wazi kuwa serikali ya sasa, iko tayari kuona nchi ikiangamia lakini Ibaki madarakani.
Hata baada ya kueleza haya yote, bado pande hizo mbili hazikukubaliani, hivyo inategemewa duru la pili la mazungumzo haya wiki ijayo huenda likaleta mabadiliko...Lakini ni mabadiliko tu na sio suluhu...
Sana sana mataifa ya magharibi yatataka kuleta suluhu ndogo ndogo za kumaliza ghasia iliyopo ili na wao waonekane wameshughulika..lakini ukweli ni kwamba mzizi wa tatizo bado haujashughulikiwa...
Kitendo cha kuwa na vikundi vyenye ikitikadi kama Al qaeda nchini Syria kunaipa nguvu serikali ya Syria, kudai zaidi kudhibitiwa kwa makundi haya zaidi ya uongozi uliopo. Vita iliyopo Syria inamapana yake. Zaidi ya itikadi za kidini zinazoizunguka..lipo swala la mataifa rafiki na ambayo sio rafiki wa Syria. Kumbuka yapo mataifa yanaoisaidia upinzani nchini Syria kwa kuwapatia fedha na silaha...wapo walio upande wa Serikali...lakini je? hawa wamekaa na kuzungumza? Ni kama mfano wa mashine inayoendeshwa na mwenzako kwa remote...halafu wewe unajitahidi kuirekebisha manually... kabla hujaidhibiti ile remote...unadhani utafanikiwa kweli?
Toa maoni yako...