BOKO HARAM NI SHIDA NIGERIA

0
Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.

Wanaume hao waliokuwa wamejihami , waliwasimamisha madereva na kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari yao kabla ya kuwapiga risasi na kuwaua.

Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na serikali kutaka utawala wa kiisilamu.

Kundi hilo huwalenga raia na wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na jeshi la taifa.








Shambulizi la hivi karibuni, lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji wa Logumani, ambao hauko mbali sana na mpaka na Cameroon.

0 comments: