WANAWAKE WANG'AA SIASA ZA CHILE

0
Nchi ya chile, ijulikanayo kama jamhuri ya chile, ni nchi katika bara Marekani ya kusini iliyopo katikati ya milima andes. Bahari ya Pasifiki upande wa Magharibi.Inapaka na na nchi ya Peru Kaskazini, Bolivia kaskazini Mashariki na Argentina upande wa mashariki.

Chile inatarajiwa kuafanya chaguzi za Urais kwa mara nyingone Desemba mwaka huu baada ya Chaguzi walizofanya jana kutokidhi mahitaji ya Katib aya nchi hiyo inayomtaka Rais apate zaidi ya Nusu ya kura zote.

Michelle Bachelet Mgombea wa kisoshalisti alimpita mwenzake kwa kupata asilimia 46.5 ya kura zote huku mwenzake Evelyn Matthei wa akiwa mwanamke wa kwanza kuwa rais mwaka 2006 mpaka 2010.
sdasa anatafuta nafasi ya pili...

Michelle Bachelet

Mpinzani wake mkubwa Evelyn Matthei, ambaye alikuwa waziri katika serikali ya mrengo w akulia ya rais Sebastian Pinera, alipata asilimia 25%.



Evelyn Matthei
Wagombea hawa wawili wa Kiti cha Urais Nchini Chile ni wanawake. Hi ni nafasi ya juu zaidi ya utawala na katika histiria nafasi hii sasa imegombewa na wanawake pekee katika nchini ya kihafishina inayoshikilia misingi na misimamo fulani fulani sio kitu kirahisi kutokea. Wadadisi wa Mambo wanahoji iwapo hii ni inaashiria ukombozi wa wanawake nchini Chile.

Lakini sio kweli kiasi kuwa ukombozi wa wanawake umefika nchini Chile ... kwani hata Nchini Marekani sio kwamba ubaguzi wa Rangi ulikwisha baada ya Rais Obama kuwa Mweusi aliyeshika madaraka nchini Humo. Lakini katika dunia ambayo wanawake wamekuwa wakidharaulika na kwekwa nyuma katik anafasi nyeti za utawala huend ahii ikaashiria mwanzo wa mabadiliko makubwa nchini Chile.


Bara la Marekani ya kusini inaendelea na mtindo wake wakutengeneza Historia pale ambapo nchjin Nyingi za bara hilo zinakuwa na viongozi wanakwake katika nafasi z ajuu za Utalwa ikiwemo nafasi ya Urais. Inachukua nafasi ya Pili baada ya Ulaya ikiwa na Takribani asilimia 23 ya wanawake katika Mabunge ya nchi hizo.

Hivi sasa Marekani ya Kusini inajumla ya viongozi wanawake watano akiwemo Dilma Rousseff wa Brazil, Cristina Fernández de Kirchner wa Argentina, Laura Chinchilla wa Costa Rica, Kamla Persad-Bissessar wa Trinidad and Tobago, na Portia Simpson-Miller wa Jamaica. Mnamo mwezi wa 12 baada ya marudio hayo ya uchaguzi wa nchini Chile idadi itapand akufikia wanawake 6.iwapo Michelle Bachelet, au Evelyn Matthei atakua RAIS.

WAKATI watu NCHI NYINGINE na kwengineko duniani hili linaweza kuonekana kama ishu ya ajabu, nchini Chile ni kitu ambacho kimekwisha anza kuzoeleka...

Mmoja wa wahombea hawa Bachelet hivi katribuni alinukuliwa akisema kuwa kwa mtu kuelezea wagombea hao kama ni wanawake pekee tayari amekwisha kuwa mbaguzi wa jinsia kwani yeye hajawahi kusikia mtu akisema Ni wanaume tu wanaogombea Urais. Mbona hiyo ya Wanaume isiwe kitu cha kuwazungumzia kw ajinsia yao..alohijo mwanamama huyu...

Aliendelea kuelezea kuwa, iwapo ni wanaume wanagombea kiti hicho...basi maswala ya maana ndiyo huzunguziwa lakini ikiwa ni wanawake basi kinachozungumziwa ni kuhusu jinsia yao...Aliendelea kusem akuwa hii sio sahihi.

Wenyewe wanasema Like Father like Daughter....

Baba za Wanawake hawa.. Bachelet and Matthei walikuwa magenerali katika kikosi cha anga cha
Chile na walikuw amarafiki wa karibu sana. Lakini baada tu ya Utawala wa Dikteta Augusto Pinochet, marafiki hawa walijikuta katika Pande tofauti na kuw ana uhasama mkubwa.

Wagombea hawa naoa wakazaliwa na kukua kila mmoja akifuata nyayo na misingi ya mzazi wake na wenyewe kujikuta masimu wakubwa...

Bachelet alijihusisha na kikundi cha kupinga utawala chile na akafungwa mwaka 1975 akiwa na mama yake.

Ni kweli kwamba licha ya kuwa wanawake wagombea hawa wanamitazamo mizuri na tofauti sana kwa nchi ya Chile...Katika mtazamo huu.

JINSIA ZAO...HAZINA NAFASI...


0 comments: