7 WAFARIKI DUNIA LEO KATIKA AJALI MIOROGORO
0
Watu
saba wamefariki dunia papo hapo leo asubuhi na wengine watano
wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wanasafiria aina ya Noah
kugongana uso kwa uso na lori la mizigo maeneo ya Dakawa mkoani
Morogoro.
Akithibitiha
kutoka kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustine
Shilogile amesema ajali hiyo imetokea baada ya Noah kujaribu kulipita
gari hilo ndipo lilipogongana uso kwa uso na Lori ambapo watu
waliopoteza maisha walikuwa kwenye Noah.
Mkuu
wa Wilaya ya Morogoro Anthony Mtaka akizungumza kutoka kwenye eneo la
tukio amewataka madereva kufuata sheria za barabarani ili kuepusha
ajali kama hizo zisizokuwa za lazima zinazogharimu maisha ya watu
pamoja na mali.